Nawaomba radhi wasomaji wote wa blog hii ya michezo.
Kumekuwa
na matatizo makubwa ya upatikanaji wa blog hii kuanzia jana, hali ambayo imetokana
na wavamizi wa mtandao kutengeneza virusi vinavyosababisha usumbufu
mkubwa kwa wasomaji wakiwatisha kuwa ukiifungua blog hii, kompyuta au
simu yako itapata matatizo.
Hali
hiyo inaendelea kufanyiwa kazi na wataalamu mbalimbali wakiwemo wale wa
Google ambao wamejua kinachofanyika. (Nashukuru Google).
Imani yangu, mambo yatakaa vizuri kuanzia leo au kesho.
Nawaomba radii kwa usumbufu wowote uliojitokeza kwenu na ambao utaendelea kujitokeza.
Kawaida
washambulizi hao, huangalia blog zinazosomwa zaidi na kufanya hivyo.
Lakini naamini mchango wenu umekuwa mkubwa hadi umewafanya kusikia wivu,
lakini juhudi zetu, zitazaa matunda na muendelee kufaidi habari murua
za kispoti na burudani kidogo.
Kwa mara nyingine, natoa shukurani kwenu na kuwaomba muendelee kuwa wavumilivu wakati kazi ya marekebisho ikiendelea.
Ahsante
KASSIM OMARY
Founder and Owner of kiungomshambuliaji BLOG.
0 Maoni:
Post a Comment