Arsene
Wenger amethibitisha kuwa atakubali Mashitaka ya FA, Chama cha Soka
England, ya Utovu wa Nidhamu yaliyotokana kumkashifu Refa na pia
kumsukuma Refa wa Akiba baada ya kuamriwa kutoka nje ya Uwanja na Refa.
Jumapili
iliyopita kwenye Mechi ambayo Arsenal iliifunga Burnley 2-1, Wenger
alimsukuma Refa wa Akiba Anthony Taylor mara tu baada ya kuamriwa na
Refa wa Mechi hiyo Jon Moss kutoka nje ya Uwanja kwa kumkashifu ikidaiwa
alimwita ‘laghai’.
Wenger
alitupwa nje ya Uwanja Dakika ya 93 mara baada ya Burnley kupewa Penati
ambayo walisawazisha Bao na Gemu kuwa 1-1 lakini Dakika chache baadae
Refa huyo huyo, Jon Moss, ndie aliwapa Arsenal Penati tata na kufunga
Bao lao la ushindi katika Dakika ya 98.
Mara baada ya Mechi hiyo, Wenger, mwenye Miaka 67, aliungama na kuomba radhi.
FA ilimpa hadi Leo Alhamisi Saa 3 Usiku, Saa za Bongo, kujibu Mashitaka yake.
Sasa Wenger amesema hatapinga Mashitaka hayo na kuiachia FA impe Adhabu.
Mwaka
2012, Meneja wa Newcastle wakati huo, Alan Pardew, alitwangwa Faini
Pauni 20,000 na kufungiwa Mechi 2 kwa kumsukuma Refa Msaidizi, Mshika
Kibendera.
Akiongea hapo Jana, Wenger alieleza: “Nipo England kwa Miaka 20 na nimeona mengi na nyinyi mnajua.”
Alipohojiwa kuhusu Adhabu anayotegemewa kupewa, Wenger alisema: “Sitegemei kitu. Niliongea baada ya Mechi ile.”
Licha
ya kutoboa kwamba atakubali Mashitaka, Wenger pia alisema ataomba yeye
mwenyewe aende kujieleza mbele ya Jopo litakalojadili Kesi yake.
0 Maoni:
Post a Comment