MCHEZAJI
wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher ambae sasa ni Mchambuzi mahiri
wa Soka huko England amedai anahofia Msimu wa Liverpool kusambaratika
mara baada ya Juzi kufungwa 1-0 na Southampton huko Anfield kwenye Mechi
ya Pili ya Nusu Fainali ya EFL CUP na kutupwa nje.
Katika Mechi ya Kwanza ya Nusu ya Kombe hilo la Ligi, Liverpool pia ilifungwa 1-0 na Southampton huko Saint Mary.
Tangu
Novemba ambapo Kikosi cha Liverpool chini ya Meneja Jurgen Klopp, baada
ya kuongoza EPL, Ligi Kuu England, kimekuwa kikiporomoka polepole na
sasa wapo Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 10 nyuma ya Vinara Chelsea.
Liverpool
wameshinda Mechi 1 tu kati ya 7 walizocheza Mwaka huu 2017, na huo ni
ushindi wa 1-0 dhidi ya Timu hafifu ya Daraja la Ligi 1 Plymouth
waliporudiana kwenye Raundi ya 3 ya FA CUP baada ya Sare yao ya 0-0 huko
Anfield.
Mechi zijazo kwa Liverpool ni dhidi ya Wolves kwenye Raundi ya 4 ya FA CUP na kisha na Chelsea kwenye EPL.
Carragher anahisi kipigo chochote kati ya hizo Mechi 2 kitaumaliza kabisa Msimu wao.
Ameeleza: “Wakiendelea kama hivi basi Msimu wao wowote utatoka nje ya Dirisha!”
Gwiji huyo amesema wakishindwa kumaliza nje ya 4 Bora kwenye EPL lawama zote atatupiwa Klopp.
LIVERPOOL – Mechi zijazo:
**EPL isipokuwa inapotajwa
- 28 Januari – Wolverhampton (FA CUP – Nyumbani)
- 31 Januari - Chelsea (Nyumbani)
- 4 Februari - Hull (Ugenini)
- 11 Februari – Tottenham (Nyumbani)
- 27 Februari – Leicester City (Ugenini)
0 Maoni:
Post a Comment