Timu
ya Stand United ya Shinyanga, imetamba kumsimamisha Mnyama leo Ijumaa
wakati timu hizo zitakapokutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara katika
Uwanja wa Taifa, Dar huku Simba ikilazimika kushinda ili kuendeleza
matumaini yake ya kutwaa ubingwa huo msimu huu.
Stand
United inayoshika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara,
imejipanga vilivyo kuwasimamisha Simba waliopo nafasi ya pili ambao
wanakimbizana na Yanga kuwania ubingwa.
Ofisa
Habari wa Stand United, Deokaji Makomba, amesema kuwa japokuwa
walikumbwa na changamoto ndogondogo za kiuchumi kipindi cha mzunguko wa
kwanza ila sasa wamejipanga vizuri kuondoka na pointi tatu kwani ni
muhimu kwao.
“Hali
ya vijana ipo vizuri na kila mchezaji amejipanga kuwakabili Simba,
tunajua mchezo huu utakuwa wa vuta nikuvute, sisi tunazitaka pointi tatu
na hata wapinzani wetu hivyohivyo wanazitaka pointi hizo, lakini kwa
jinsi tulivyojipanga ni lazima tuwasimamishe Simba kwa kuwachapa,”
alisema Makomba.
0 Maoni:
Post a Comment