LEO
Chelsea wapo The Hawthorns kucheza na West Bromwich Albion wakijua
ushindi kwao utawapa Ubingwa wa EPL, LIGI KUU ENGLAND huku wakiwa na
Mechi 2 mkononi.
Chelsea
wanaongoza Ligi hii wakiwa na Pointi 84 kwa Mechi 35 wakibakiza Mechi 3
na Timu pekee inayoweza kuwakamata ni Tottenham Hotspur ambao wana
Pointi 77 kwa Mechi 35.
Ikiwa Chelsea watashinda hii Leo watafikisha Pointi 87 ambazo Tottenham hawawezi kuzifikia.
Hii
Leo Chelsea wanacheza na WBA ambayo waliifunga katika Mechi ya Kwanza na
ambayo ipo Nafasi ya 8 ikiwa salama salimini kwenye vita ya kujinusuru
kushuka Daraja.
Kila Timu inatarajiwa kuwa na Kikosi kamili na Kiungo wa Chelsea, N'Golo Kante, anatarajiwa kucheza baada ya Jumatatu iliyopita kuikosa Mechi na Middlesbrough akiwa na maumivu ya Paja.
Kante
ndie ambaye ametwaa Tuzo za Mchezaji Bora zilizotolewa na PFA na FWA,
Vyama vya Wachezaji wa Kulipwa na kile cha Waandishi wa Soka.
Mechi nyingine ya EPL hii Leo ni huko Goodison Park kati ya Everton na Watford.
EPL, LIGI KUU ENGLAND
Ratiba:
Ijumaa Mei 12
2145 Everton v Watford
2200 West Bromwich Albion v Chelsea
Jumamosi Mei 13
1430 Manchester City v Leicester City
1700 Bournemouth v Burnley
1700 Middlesbrough v Southampton
1700 Sunderland v Swansea City
1930 Stoke City v Arsenal
Jumapili Mei 14
1400 Crystal Palace v Hull City
1615 West Ham United v Liverpool
1830 Tottenham Hotspur v Manchester United
0 Maoni:
Post a Comment