Pambano la Ligi Kuu
baina ya Yanga na Mbeya City litachelewa kuanza kwa masaa mawili kinyume
na utaratibu wa kawaida wa mechi za Dar kuchezwa kuanzia saa kumi.
Mchezo huo utaanza
majira ya saa 12:00 jioni na hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa klabu hiyo
kongwe kabisa nchini kucheza mchezo wake wa ligi kuu usiku katika miaka
ya hivi karibuni.
Taarifa rasmi ya klabu hio imesema,
“Maamuzi haya
yamezingatia matakwa na masilahi ya wadau wa soka nchini ambao wana kiu
na hamu ya kuutazama mchezo huo lakini pia wakiwa ni sehemu ya wadau wa
mchezo wa riadha itakayofanyika uwanja wa taifa jumamosi hiyo hiyo.
Tunawaomba wanachama na mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwapa sapoti vijana wao kwani ulinzi utakuwa imara na thabiti. ”
0 Maoni:
Post a Comment