Uongozi wa klabu ya LA Galaxy ya marekani umedai kwamba kwa sasa
una mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Manchester United Zlatan
Ibrahimovic kwa dau kubwa liltakalo mfanya awe ndio mchezaji ghali
zaidi wa kulipwa katika Ligi Kuu ya soka ya marekani.
Ibrahimovic alijiunga na United kwa mkataba wa mwaka mmoja msimu mfupi uliopita.
Lakini
hata hivyo ni maamuzi ya hiari kwa msweeden huyo ya kuchagua kuondoka
au kubakia endapo United watahitaji kufanya mazungumzamo na mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka kwa 35.
Mpaka sasa Ibrahimovic
aimefunga mabao 26 United katika msimu huu, leo Alhamisi
atakosa mchezo wa Uefa Europa ligi dhidi ya Rostov kutokana na
kutumikia adhabu ya mechi tatu hii ni baada ya kuadhibiwa kutokana
na makosa aliyoyafanya kwenye mchezo dhidi ya Bournemouth kwa
kumchezea madhambi Tyrone Mings siku ya Jumamosi iliyopita katika
uwanja wa Old Traford.
0 Maoni:
Post a Comment