Mechi za Pili za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, zinaanza kuchezwa Jumanne Machi 7 kwa Mechi 2.
Siku
hiyo, huko Emirates Jijini London, Wenyeji Arsenal wanapaswa kupindua
kipigo cha 5-1 walichoshushiwa na Bayern Munich katika Mechi ya Kwanza
iliyochezwa huko Germany.
Ili
kufuzu kuingia Robo Fainali, Arsenal wanapaswa kitu ambacho hakijawahi
kufanyika kwenye UCL kwa kushinda 4-0 ama kwa idadi nyingine ya Mabao
ili mradi tofauti ya Magoli iwe 4-0.
Mechi
ya Pili ya Jumanne ni huko Naples, Italy wakati Napoli ikirudiana na
Mabingwa Watetezi Real Madrid huku wakihitaji ushindi wa Bao 2-0 kwa
vile walichapwa 3-1 huko Santiago Bernabeu Jijini Madrid, Spain kwenye
Mechi ya Kwanza.
Napoli pia wanaweza kufuzu ikiwa watashinda kwa idadi nyingine ya Mabao ili mradi tofauti ya Magoli iwe 2-0.
Jumatano Machi 8 zipo Mechi nyingine 2 za Pili za
Raundi ya Mtoano ya Timu 16 kati ya Barcelona na Paris Saint Germain
huku PSG wakiwa mbele 4-0 na ya pili ni kati ya Borussia Dortmund na
Benfica huku Benfica wakiongoza 1-0.
Mechi za Pili za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 zitakamilika Wiki ijayo, Machi 14 na 15, kwa Mechi nyingine 4 ili kutoa Washindi watakaocheza Robo Fainali.
0 Maoni:
Post a Comment