IMERIPOTIWA
kuwa Alexis Sanchez aligombana na Wachezaji wengine katikati ya Mazoezi
yao kuelekea Mechi yao ya Jumamosi waliyotandikwa 3-1 na Liverpool huko
Anfield ikiwa ni Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
Imedaiwa Sanchez, Mchezaji kutoka Chile mwenye Miaka 28, alizongwa na wenzake huku mmoja wao akizuiwa ‘kumpiga’.
Baada
ya sakata hilo, Meneja wa Arsenal Arsene Wenger hakumuanzisha Sanchez
kwenye Mechi na Liverpool akidai ni sababu za kimbinu tu na badala yake
kuwatumia Danny Welbeck na Olivier Giroud akieleza kuwa hao ni wazuri
kwenye Mipira ya juu akimaanisha Arsenal walitaka kutumia mbinu ya
Mipira Mirefu na ya juu kuifyeka Liverpool.
Lakini
Wenger akamuingiza Sanchez baada ya Haftaimu na Mchezaji huyo kutoa
Pasi kwa Danny Welbeck aliefunga Bao pekee la Arsenal kwenye Mechi hiyo
na Liverpool.
Msimu huu, Sanchez ameshiriki kwenye Bao 26 za Arsenal yeye akifunga 17 na kusaidia 9.
Mbali ya vurumai hizo, yapo madai Sanchez hataki kuongeza Mkataba na anataka kuhama mwishoni mwa Msimu huu.
Kipigo hicho cha Liverpool ni cha 3 kwa Arsenal katika Mechi zao 4 za Ligi zilizopita.
0 Maoni:
Post a Comment