EPL: SPURS, CITY ZAJICHIMBIA NAFASI ZA 2 NA 3.

  Tokeo la picha la sunderland vs man city image

Tottenham na Manchester City zimejichimbia Nafasi za Pili na za 3 EPL, Ligi Kuu England, baada ya jana kushinda Mechi zao za Ligi hiyo.
 
Spurs, wakicheza kwao White Hart Lane, waliifunga Everton 3-2 na kujiweka vizuri Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 56 kwa Mechi 27 huku kileleni wapo Chelsea wenye Pointi 63 kwa Mechi 26.

Bao za Mechi hiyo zilifungwa Dakika za 20 na 56 kwa Bao za Harry Kane na la 3 Dakika ya 92 kupitia Dele Alli huku Everton wakipiga Bao zao 81 na 93 Wafungaji wakiwa ni Romelu Lukaku na Enner Valencia.

Huko Stadium of Light, Sunderland wamebaki mkiani baada ya jana kuchapwa 2-0 na Man City kwa Bao za Sergio Aguero na Leroy Sane.

Ushindi huu umewaweka Man City Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 55 kwa Mechi 26.
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment