Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania bara Yanga, jana
wameshindwa kuing'oa vinara wa ligi hiyo Simba baada ya kutoka Sare
ya 0-0 na Mtibwa Sugar Jamhuri Mjini Morogoro.
Yanga wangeweza
kushinda Mechi hii baada ya kupewa Penati ya Dakika ya 34 lakini
Mchezaji wao Simon Msuva akashindwa kuifunga Penati hiyo.
Kwa
Matokeo hayo Yanga wanabaki Nafasi ya Pili nyuma ya Simba ambao wako
alama 2 mbele yao baada ya Jumamosi kutoka Sare 2-2 na Mbeya City.
Katika Mechi nyingine iliyochezwa jana African Lyon iliitungua Mwadui FC 1-0 .
Ligi
hiyo ya Tanzania bara inatarajia kuendelea tena leo Jumatatu Machi 6 kwa
mchezo mmoja ambapo Ndanda wanakuchele wanawakaribisha maafande wa
Ruvu Shooting.
0 Maoni:
Post a Comment