Mshambuliaji
Mtanzania, Mbwana Samatta ameendelea kuonyesha ni mtu “hatari” baada ya
kufunga mabao mawili wakati timu yake ya Genk ikishinda kwa mabao 2-1
dhidi ya Club Brugge.
Katika
mechi hiyo ya Ligi Kuu Ubelgiji, wageni Brugge walionekana ni hatari
dakika za mwanzo, lakini dakika ya 5 tu, Samatta akawatuliza kwa kufunga
bao la kwanza akipokea pasi ya Ruslan Malinovsky.
Samatta
alirejea tena kambani katika dakika ya 42 akifunga baada ya kupokea
pasi ya Pozuelo na Brugge wakafunga bao lao pekee dakika ya 43
kupitia Jose Izquierdo.
Nahodha huyo wa Taifa Stars, alipumzishwa katika dakika ya 85 baada ya kuwa amemaliza kazi yake hiyo muhimu
0 Maoni:
Post a Comment