LICHA
kulaumiwa mno kwa uamuzi wake wa kumpiga Benchi Staa wake Alexis
Sanchez kwenye Mechi Arsenal waliyotwangwa 3-1 hapo Jana huko Anfield na
Liverpool, Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ametetea uamuzi wake huo wa
kutomuanzisha Sanchez.
Wakiwa
2-0 nyuma, Wenger alimuingiza Sanchez wakati wa Haftaimu na yeye ndio
alietoa Pasi ambayo Danny Welbeck aliifungia Arsenal Bao lao Moja.
Msimu huu, Sanchez ameshiriki katika Bao 26 za Arsenal akifunga 17 na kusaidia 9.
Baada ya Mechi hiyo, Wenger alieleza: “Kila Mtu ana maoni yake. Mie nina nguvu na ujuzi wa kujua nini matokeo ya uamuzi ule!”
Kwenye Mechi ya Jana, badala ya kumtumia Sanchez, Wenger aliamua kuwaweka pamoja Welbeck na Oliver Giroud.
Ameeleza: “Nilitaka kuwaanzisha Wachezaji ambao ni wazuri kwa Mipira ya juu na kisha kumuingiza Sanchez Kipindi cha Pili.”
Wenger amekiri uamuzi wa kumpiga Benchi Sanchez haukuwa rahisi.
Kipigo
cha Liverpool ni cha 3 kwa Arsenal katika Mechi zao 4 za Ligi
zilizopita na kuwatupa Nafasi ya 5 kwenye Ligi wakiwa Pointi 2 nyuma ya
Timu ya 4 Man City ambao wana Mechi 1 mkononi.
MARTIN KEOWN, Beki wa zamani wa Arsenal, akiongea na BBC alisema: “Kumpiga
Benchi Sanchez kulishtua! Sielewi ni kwanini. Yeye ndie Mchezaji wao
Bora! Sikumbuki katika Miaka 20 ya Wenger wakicheza Soka bovu lilikosa
ari na moyo kama lile!”
0 Maoni:
Post a Comment