Wezi wanaaminika kuvunja na kuingia
katika nyumba ya aliyekuwa nahodha wa timu ya uingerewza John Terry
wakati akiwa katika likizo ya kifamilia.
Maafisa wa polisi wa Surrey walithibitisha kwamba nyumba iliopo Oxshott ilivunjwa wikendi iliopita.
John Terry ameripotiwa kuishi katika nyumba ya vyumba saba nchini humo.
Msemaji
wa kituo hicho cha polisi wa Surrey amesema kuwa : Tunaweza
kuthibitisha kuwa wizi ulifanyika katika nyumba moja iliopo Moles Hill
,Oxshott usiku wa terehe 25 na 26 mwezi Februari.
Wezi hao
wanadaiwa kuvunja na kuingia katika nyumba hiyo na kuiba vitu vyenye
thamani wakati ambapo mchezaji huyo wa Chelsea mwenye umri wa miaka 36
alikuwa ameenda likizo na watu wa familia akiwemo mkewe Toni kulingana
na ripoti za gazeti la The Sun.
0 Maoni:
Post a Comment