Timu ya Kenya ya raga (RUGBY) ya wachezaji
saba kila upande imejinyakulia taji la trophy mjini Las Vegas baada ya
kuishinda Samoa 21-14 katika fainali iliochezwa uwanja wa Sam Boyd.
Ni
kombe la pili la timu ya shujaa baada ya kushinda kombe kama hilo
katika mashindano ya Wellington sevens mnamo mwezi Januari 29.
Nahodha
Andrew Amonde aliongoza kikosi hicho baada ya kufunga trai mbili huku
Collins Injera akiongeza trai nyengine kwa kupiga mkwaju wa sammy Okoth.
Ikielekea fainali Kenya iliicharaza Ufaransa 14-7 huku samoa ikiishinda Scotland 24-0 katika semi.
Amonde alikuwa na haya ya kusema: Hatukecheza vyema sana lakini ni vizuri kupata kitu.
Nashukuru mashabiki, tunajua tuna zaidi na tutategemea ushindi huo huko mjini Vancouver.
Nyota
mwenye kasi zaidi Injera alipata mpira na kuipita safu ya ulinzi ya
Samoa kwa trai yake ya 242 huku Olich akifunga na kuiweka Kenya kifua
mbele 7-0.
0 Maoni:
Post a Comment