Baada ya kupata ushindi katika pambano lake dhidi ya bingwa wa
zamani wa uzito wa juu bondia David Haye ,bondia Tony Bellew amesema
yawezekana ikawa ndio muda wake wa kuamua kupumzika kuendelea na
mchezo huo.
David Haye na bondia Tony Bellew walipigana katika pigano lililofanyika jumamosi kwenye ukumbi wa O2 Arena, Jijini London.
Katika
mchezo huo Haye alionekana kushindwa kusimama vyema kutokana na kuumia
vibaya mguu wake wa kulia, lakini alipambana hadi raundi ya 11 pale
kambi yake ilipoamua kutupa taulo jeupe ili kuomba kumalizwa kwa pambano
hilo.
Bondia David Haye amelazimika kufanyiwa upasuaji wa msuli
nyuma ya mguu ni mara baada ya kuumia katika pambano lililomkutanisha
dhidi ya bondia Tony Bellew huko London.
Katika pambano hilo David
Haye aliumia misuli ya mguuni katika raundi ya sita na hivyo kujikuta
akipigwa vikali na kushindwa kuendelea na pambano katika raundi ya 11.
Mara
baada ya kufanyiwa upasuaji huo mwakilishi wa David amewashukuru wale
wote waliomtumia ujumbe wa pole na kumtia nguvu, pamoja na jopo la
madaktari kutoka katika hospitali waliyomfanyia upasuaji.
Kwa upande wake Tony Bellew amesema alivunjika mkono katika pambano hilo japo alikuwa hasikii maumivu hata kidogo.
Amesema
alivunjika mkono huo katika raundi ya pili au raundi ya tatu katika
mahojiano maalum na Shirika la Utangazaji Uingereza BBC.
0 Maoni:
Post a Comment