KWA
MARA NYINGINE tena Arsenal wanachungulia kutupwa nje ya Hatua ya Raundi
ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, hatua ambayo mara ya
mwisho waliivuka Msimu wa 2009/10.
Kibarua
kigumu cha Arsenal kinatokana na kuchapwa 5-1 na Wababe wa Germany
Bayern Munich kwenye Mechi yao ya Kwanza iliyochezwa Allianz Arena huko
Munich.
Ili
kusonga Robo Fainali, Arsenal wanahitaji ushindi wa 4-0 au matokeo
mengine ili mradi tofauti ya Magoli ibakie 4-0 kwa upande wao.
Kazi hii ngumu ipo ngumu zaidi kwao kwa vile pia watamkosa Kiungo wao Mjerumani Mesut Ozil ambae ni Mgonjwa.
Lakini
Arsenal wanaweza kumtumia kwa mara ya kwanza Sentahafu wao Mjerumani
Per Mertesacker ambae ni Kepteni wao baada ya kupona Goti na hii itakuwa
Mechi yake ya kwanza kucheza Msimu huu ikiwa atacheza.
Pia
huenda Meneja wa Arsenal Arsene Wenger huenda akamuanzisha Fowadi wao
kutoka Chile Alexis Sanchez ambae hakuanza Jumamosi iliyopita
walipotwangwa 3-1 na Liverpool huko Anfield kwenye Mechi ya Ligi Kuu
England baada kuvumishwa kulikuwa na rabsha Mazoezini iliyomhusu yeye.
Sanchez ndie Mfungaji Bora wa Arsenal Msimu huu akiwa na Bao 20.
Kwa
upande wa Bayern Munich, chini ya Kocha Mtaliano Carlo Ancelotti,
itawakosa Jerome Boateng ambae ni Majeruhi na Philipp Lahm ambae yupo
Kifungoni.
JE WAJUA KUELEKEA MECHI YA ARSENAL VS B. MUNICH?
- Arsenal na Bayern zimekutana mara 11 na 7 kati ya hizo ni katika Miaka Minne iliyopita.
- Bayern imeshinda Mechi 6 na kufungwa 3 tu kati ya hizo huku wakiipiga Arsenal 5-1 mara 2 mfululizo katika Mechi 2 zilizopita.
Pengine
matumaini makubwa kwa Arsenal ni kuwa Bayern imepigwa mara 2 mfululizo
kila walipotua England katika Mechi 2 zilizopita na ya mwisho ikiwa Emirates walipochapwa 2-0 na Arsenal kwa Bao za Olivier Giroud na Mesut Ozil.
Lakini
Bayern watatua Emirates wakiwa hawajafungwa katika Mechi 16 huku
wakishinda Mechi 14 kati ya hizo mbio zilizoanzia Novemba Mwaka Jana.
Katika Mechi zao 5 zilizopita, Bayern wamenyuka Bao 20.
0 Maoni:
Post a Comment