Kocha Mkuu wa Mbeya City, Kinnah Phiri ameendelea kusisitiza kuwa kikosi chake sasa kina nafasi ya kuamka na kufanya vema.
Baada
ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Simba huku Mbeya City ikionyesha soka
safi, Phiri raia wa Malawi amesema anaamini kikosi chake kitafanya vema.
“Morali imepanda na si kwamba wachezaji hawanielewi lakini mchezo wa soka unajumuisha mambo mengi sana,” alisema.
“Sasa ninaamini wataweza kucheza kwa kiwango hicho na baada ya hapo kuendelea kukipandisha,” alisema.
Kabla, Mbeya City ilikuwa inasuasua kwa kiasi kikubwa licha ya juhudi ya usajili mzuri.
0 Maoni:
Post a Comment