LIVERPOOL
wameambiwa kinagaubaga na FIFA waamue wenyewe kama Mchezaji wao Joel
Matip anaweza kuichezea Timu hiyo baada ya kukataa kujiunga na Cameroon
kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2017, yanayoendelea
huko Gabon hivi sasa.
Liverpool
waliamua wenyewe kumtoa Matip Kikosini Jumapili walipocheza huko Old
Trafford na Manchester United kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England,
wakidai wanangoja ufafanuzi wa FIFA.
Hapo jana FIFA imetoa ufafanuzi na kuitaka Liverpool kufuata Kanuni
zinazohusu Wachezaji na moja ikiwa ile inayotaka Mchezaji anaeitwa na
Nchi yake kuichezea Timu ya Taifa kutoichezea Klabu yake katika kipindi
hicho.
Liverpool
imekuwa ikidai Matip hakuwemo kwenye Kikosi cha mwisho cha AFCON 2017
na kabla alishatangaza kuachana na kuichezea Cameroon.
Hata
hivyo, Liverpool wameshindwa kumtumia Matip kwenye Mechi zao na
kumwacha Meneja wao Jurgen Klopp akilalamika baada ya Shirikisho la Soka
la Cameroon, FECAFOOT, kukaa kimya na kutojibu maombi ya Liverpool ya
kutaka ufafanuzi na uthibitisho.
FIFA
pia hii Leo imefafanua kuwa Chama cha Soka cha Nchi kikitaka kumwita
Mchezaji kwa ajili ya Mashindano ya Fainali za Kimataifa inapaswa
kumjulisha Mchezaji anaehusika kwa Maandishi si chini ya Siku 15 kabla
Siku anayopaswa kujiunga rasmi na Nchi yake na Taarifa hiyo pia inapaswa
kupelekwa kwa Klabu ya Mchezaji huyo katika muda huo huo.
FIFA pia imesisitiza kukiukwa kwa Kanuni hizo kutafanya Wahusika kuburuzwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ya FIFA.
Hadi sasa haijulikani kama FECAFOOT ilitoa rasmi Notisi hiyo ya Siku 15 kwa Matip na Liverpool.
0 Maoni:
Post a Comment