Mshambuliaji
nyota Mtanzania, Mbwana Samatta ameonyesha kweli ni moto baada ya
kufunga mabao mawili wakati timu yake ikishinda kwa mabao 5-2 ugenini
dhidi ya Gent.
Genk imeichapa Gent, zote za Ubelgiji kwa mabao 5-2 katika mechi ya raundi ya 16 Bora Europa Cup, kuwania kwenda robo fainali.
Samatta
ambaye watangazaji wengi wa runinga barani Ulaya wamekuwa wakitamka
jina lake “Bwana Samatta”, alianza kufunga katika dakika ya
41, likiwa bao la tatu.
Kabla
Ruslan Malinovsky alikuwa amefunga bao kwa mkwaju wa adhabu katika
dakika ya 21 na Gent wakasawaisha kupitia kinda Mnigeria, Samuel Kalu
katika dakika ya 27.
Omar
Colley raia wa Gambia akaongeza bao la pili dakika ya 33 kabla ya
Samatta kufunga na Jere Uronen akafunga la nne kabla ya kwenda
mapumziko.
Gent
ambao walikuwa nyumbani walianza kipindi cha pili kwa kasi na
kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 61 kupitia Kalifa Coulibaly.
Wakati
Gent wanaona mambo yanaenda vizuri, Genk wakaamka na Samatta akapigilia
msumari wa tano katika dakika ya 72 akiunganisha krosi safi ya Thomas
Bufel.
0 Maoni:
Post a Comment