Manyika anatarajiwa kuondoka Simba baada ya baba yake
kumwahidi kumtafutia timu nyingine sababu ya kukosa nafasi kwenye
kikosi cha Simba.
Kipa namba mbili wa Simba Manyika Peter huenda akaachana na timu hiyo
mwishoni mwa msimu huu baada ya Baba yake kumtaka kutafuta timu ambayo
atapata nafasi ya kucheza.
Manyika amesema kuwa amevumilia kwa muda mrefu lakini kwa sasa
amepoteza matumaini kutokana na maisha yake yote kuishia benchi jambo
ambalo lina mvunja moyo wa kuendelea kuichezea timu hiyo akihofia
kupoteza kipaji chake.
“Baba amenishauri mwishoni nitafute timu nyingine ya kuchezea, kwa
sababu kuendelea kubaki Simba ni sawa na kuua kipaji changu, muda mwingi
nakuwa benchi hata kwenye mechi za kirafiki kipa anayepangwa ni Mghana
Daniel Agyei,” amesema Manyika.
Kipa huyo amesema anafikiria kutekeleza ushauri wa mzazi wake kwa
sababu nikweli, kiwango chake kimekuwa kikipungua siku hadi siku jambo
linasababishwa na kutocheza mechi za ushindani ukiacha mazoezini.
Amesema kama mchezaji mdogo anandoto za kufanya vizuri na kwenye
nafasi hiyo ya langoni lakini anashangazwa na maboss zake Joseph Omog na
msaidizi wake Jackson Mayanja kumfungia vioo huku wakimsotesha benchi.
“Inauma kuona msimu umebakiza mechi sita alafu sijacheza hata mechi
moja na mbaya zaidi wageni wanakuja na kupata nafasi huku mimi
nikiendelea kuwa mchezaji wa mazoezini kwani hata mechi za Kombe la FA
au zile za kirafiki sipangwi,” amesema Manyika.
Kipa wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Peter Manyika, amesema
atamwondoa mwanawe, Manyika Peter, kudakia Simba kutokana na kukosa
nafasi katika kikosi cha kwanza cha Joseph Omog.
Manyika alijiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili ambao
unamalizika mwishoni mwa msimu huu na tayari baba yake mzazi Peter
Manyika ambaye amewahi kuichezea timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’
na klabu ya Yanga amemhakikishia kumtafutia timu ya kucheza itakayompa
nafasi ya kikosi cha kwanza.
0 Maoni:
Post a Comment