Katika viwango vipya vya ubora duniani vinavyotolewa na Shirikisho la
Soka Duniani-FIFA kila mwezi kwa sasa vimeonyesha baadhi ya mataifa
kupanda katika nafasi.
Kwa upande wa orodha ya jumla; Argentina bado
wameendelea kuwa vinara wakifuatiwa na Brazil katika nafasi ya pili huku
mabingwa wa dunia Ujerumani wakiwa nafasi ya tatu.
Kwa upande wa
Afrika ; Uganda bado wanaendelea kuongoza kwa Afrika Mashiriki wakiwa
nafasi ya 16 kwa Afrika na 74 duniani wakifuatiwa na Kenya waliopo
nafasi ya 21 Afrika na 88 duniani wakati Rwanda wako nafasi ya 24 Afrika
na 93 duniani na Burundi nafasi ya 41 Afrika na 139 duniani.
Misri
wao wameendelea kuwa vinara kwa kukwea kwa nafasi mbili zaidi hadi
nafasi ya 20, wakifuatiwa na Senegal walioko nafasi ya 28 huku mabingwa
wa michuano ya Mataifa ya Afrika Cameroon nao wakikwea kwa nafasi moja
mpaka nafasi ya 32 duniani.
Mabingwa wa Amerika Kusini Chile wapo nafasi ya nne na Ubelgiji ndio wanakamilisha tano bora kwenye orodha hizo.
Tanzania imepanda kwa nafasi moja katika viwango kwa nafasi ya 158
0 Maoni:
Post a Comment