Uongozi wa Azam FC umewaambia wapenzi na
mashabiki wa Simba na timu nyingine, waungane kwa pamoja kuishabikia
Yanga, kesho Jumamosi itakapocheza dhidi ya Zanaco ya Zambia.
Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Habari wa
Azam FC, Jaffar Idd huku akisisitiza kwamba kufanya hivyo ni uzalendo
ambao unatakiwa kuanzia sasa na kuendelea.
Yanga itacheza dhidi ya Zanaco katika
Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambapo mshindi
atacheza hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Upande mwingine, Azam FC yenyewe
itacheza dhidi ya Mbabane Swallows ya Swaziland kwenye Uwanja wa Azam
Complex, Dar, ukiwa ni mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, keshokutwa
Jumapili.
“Kwa sasa lazima tukubali tu kwamba
Yanga na Azam ndiyo wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya
kimataifa, hivyo litakuwa jambo la busara kwa mashabiki wote kuweka
itikadi zetu pembeni na kuuungana pamoja kuhakikisha timu hizi zinafika
mbali.
“Nawaomba tu mashabiki wote, wa Azam,
Simba na timu nyingine Jumamosi tukaishangilie Yanga pale Taifa, kisha
Jumapili, tuungane tena kwenda Azam Complex kuishangilia Azam,” alisema
Idd.
0 Maoni:
Post a Comment