Xavi,
Mkongwe aliechezea Barcelona kwa Miaka 17 na kuhamia Al Sadd ya Qatar
Mwaka 2015, anahisi Real Madrid itatwaa Ubingwa wa La Liga Jumapili
lakini anaona Juventus ya Italy itaibwaga Real kwenye Fainali ya UEFA
CHAMPIONZ LIGI hapo Juni 3.
Jumatano
iliyopita Real, chini ya Kocha Zinedine Zidane, iliitandika Celta Vigo
4-1 na kuongoza La Liga Pointi 3 mbele ya Barcelona huku kila Timu
ikibakiza Mechi 1 tu itakayochezwa Jumapili.
Hiyo
Jumapili Real wanahitaji Pointi 1 tu Ugenini na Malaga ili kuzoa Ubingwa
wao wa kwanza wa La Liga tangu 2012 lakini Barca wataombea yatokee yale
ya Msimu wa 1991/92 wakati Tenerife ilipoifunga Real na Ubingwa
kupeperuka kwenda Barca katika Mechi ya Mwisho ya Msimu.
Lakini Xavi, alietwaa Mataji 8 ya La Liga akiwa na Barca, amekubali kuwa safari hii Real hawawezi kuteleza.
Ameeleza:
“Ni ngumu La Liga kuiponyoka Real. Wao ni Timu imara. Wana Kiungo imara
kina Toni Kroos, Luka Modric, Isco…..nawapenda wote!”
Aliongeza:
“Malaga wapo vizuri na kuwafunga kwao ni ngumu. Wanapaswa kuleta
miujiza kama ya Tenerife ili Barca watwae La Liga. Vipigo kwa Barca
Nyumbani na Alaves na Deportivo La Coruna Ugenini vimeleta balaa kwa
Barca Msimu huu!”
Wakitwaa
La Liga, Real watakuwa njiani kutwaa Dabo kwani wapo Fainali ya UEFA
CHAMPIONZ LIGI watakayocheza na Juventus hapo Juni 3 huko Cardiff, Wales
wakiwania kuwa Klabu ya Kwanza kutetea vyema Ubingwa huu.
Lakini
Xavi anaamini Fainali hiyo ni ngumu mno na anaombea Kipa Mkongwe wa
Juve, Gianluigi Buffon, atamaliza subira yake ya muda mrefu ya kutotwaa
Kombe hili.
Xavi
ameeleza: “Juventus ni wazuri sana. Wameonyesha hilo kwa kuwatupa nje
Barca na pia wana ngome imara. Hii Fainali ni 50-50. Nilimsikia Buffon
akisema hajatwaa Kombe hili. Anastahili kulibeba pamoja na Ballon
d'Or!”.
LA LIGA:Ratiba;
Raundi ya 38 – Mechi za Mwisho
Ijumaa Mei 19
21:45 Granada v Espanyol
Jumamosi Mei 20
18:00 Deportivo v Las Palmas
18:00 Sporting Gijon v Real Betis
18:00 Leganes v Alaves
18:00 Deportivo v Las Palmas
18:00 Sporting Gijon v Real Betis
18:00 Leganes v Alaves
Jumapili Mei 21
17:45 Atletico Madrid v Athletic Club
17:45 Celta Vigo v Real Sociedad
17:45 Sevilla v Osasuna
17:45 Valencia v Villarreal
21:00 Barcelona v Eibar
21:00 Malaga v Real Madrid
17:45 Atletico Madrid v Athletic Club
17:45 Celta Vigo v Real Sociedad
17:45 Sevilla v Osasuna
17:45 Valencia v Villarreal
21:00 Barcelona v Eibar
21:00 Malaga v Real Madrid
0 Maoni:
Post a Comment