Simba wanataka kushinda mechi ya mwisho dhidi ya Mwadui FC bila kujali chochote kitakachotokea.
Ukitaka kupata uhakika wa hilo, utaona hivi, Simba wameamua kuchukua wachezaji wao wote na kwenda nao kambini.
Simba imeweka kambi Dege Beach nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kujiandaa na mechi hiyo.
“Kweli
ni kikosi chote kipo hapa kambini, tunajiandaa na mechi ya mwisho ya
Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui FC,” alisema Mratibu wa Simba, Abbas Ally
‘Gazza’.
Kabla
Simba wamekuwa wakiingia kambini na wachezaji baadhi huku wengine
wakiwa nje ya kambi hasa wale ambao wanakuwa hawatarajii kucheza.
0 Maoni:
Post a Comment