BOSI wa zamani wa Manchester United na Timu ya Taifa ya Netherlands Louis van Gaal ameamua kustaafu Ukocha baada ya kuwemo kwenye kibarua hicho kwa Miaka 26.
Van
Gaal, mwenye Miaka 65, amekuwa hana kazi tangu atimuliwe na Man United
Mwezi Mei 2016 mara tu baada ya kuiwezesha Klabu hiyo kutwaa FA CUP.
Habari
za kustaafu kwa Van Gaal zimechomoza kwenye Gazeti la huko Netherlands,
De Telegraaf, ambalo lilimnukuu akisema: “Nilidhani nitaacha nilipotoka
Man United, kisha nikasema ngoja nipumzike lakini sasa naona sitarejea
tena Ukocha!”
Uamuzi huo umekuja mara tu baada ya kupokea Tuzo ya Utumishi uliotukuka toka kwa Serikali ya Netherland.
Mbali ya Man United, Van Gaal pia aliwahi kuwa na Klabu za Ajax, Barcelona, Bayern Munich na AZ.
VAN GAAL – Tuzo kubwa Maishani mwake:
Ubingwa: Ajax (1993-94, 1994-95, 1995-96),
Barcelona (1997-98, 1998-99),
AZ Alkmaar (2008-09),
Bayern Munich (2009-10)
UEFA CHAMPIONZ LIGI: Ajax (1994-95)
Uefa Cup: Ajax (1991-92)
FA Cup: Manchester United (2015-16)
0 Maoni:
Post a Comment