YANGA KUIVAA MAJIMAJI (WANALIZOMBE) LEO.

Tokeo la picha la vodacom primier league image

VPL, Ligi Kuu Vodacom, Leo ipo huko Uwanja wa Majimaji Mjini Songea wakati Majimaji FC ikicheza na Mabingwa Watetezi Yanga.
 
Majimaji FC, chini ya Kocha Kalimangonga 'Kally' Ongala, wapo Nafasi ya 14 wakiwa na Pointi 17 wakati Yanga wapo Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 40 huku Vinara ni Simba wenye Pointi 44.
 Tokeo la picha la majimaji vs yanga image
 
Yanga, chini ya Kocha Mkuu wao George Lwandamina, walitua huko Songea tangu Juzi lakini bila ya Wachezaji wao kadhaa maarufu.
 
Wachezaji ambao hawapo Kikosini ni Beki Vincent Bossou alieko kwenye AFCON 2017 huko Gabon na Nchi yake Togo na Majeruhi Mzimbabwe Donald Ngoma pamoja na Wazambia wao Wawili Justin Zulu na Obrey Chirwa.
Pia Mchezaji wao mpya, Emmanuel Martin, ambae amepatwa na Msiba.

Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment