FIFA imethibitisha kuwa Droo za kupanga Makundi na Mechi za Fainali
za Kombe la Dunia la Mwaka 2018 huko Russia itafanyika Ijumaa Desemba 1
huko Kremlin Jijini Moscow.
Wakati Tarehe ya Droo ilikuwa ishajulikana, mahali pa kuifanyia palikuwa bado hapajatangazwa.
Kwa kuichagua Kremlin, Russia imeonyesha jinsi inavyoipa kipaumbele Fainali hizo.
Kremlin ni Ngome kubwa ya Urusi ambayo inatambuliwa na UNESCO kama
moja ya Sehemu za Urithi wa Dunia (UNESCO World Heritage Site).
Kremlin ni eneo ambalo lina Makanisa ya Kiasili na Majumba ya
Kifalme na mojawapo ni yale Makazi Rasmi ya Rais wa Urusi Vladimir
Putin.
Huko Kremlin Droo yenyewe itafanyika kwenye Jengo la Kifalme
liliokuwa likitumika kwa ajili ya Mikutano ya Chama cha Kikomunisti cha
Soviet Union na baadae kugeuzwa kuwa Ukumbi wa Burudani.
Ukumbi huo una uwezo wa kuchukua Watazamaji 6,000.
Russia walishinda Kura za kuwa Mwenyeji wa Fainali za Kombe la
Dunia za Mwaka 2018 zilizofanyika Desemba 2010 kwa kuwabwaga Wagombea
wengine ambao ni Belgium/Netherlands (Waliotaka kuwa Wenyeji wenza),
England na Portugal/Spain (Waliotaka kuwa Wenyeji wenza).
Kuanzia Juni 17 na Julai 2 Mwaka huu, Russia watakuwa Wenyeji wa
Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara, FIFA CONFEDERATION CUP, ambalo
washindani wake ni Russia, kama Mwenyeji, Mabingwa wa Dunia Germany na
Mabingwa wa Mabara 6 Duniani ambao ni Australia, Chile, Mexico, New
Zealand, Portugal na Bingwa wa AFCON 2017, Kombe la Mataifa ya Afrika
ambazo Fainali zake zinaendelea hivi sasa huko Gabon.
Ni desturi kwa Mashindano hayo kufanyika kwa Nchi Mwenyeji wa
Fainali za Kombe la Dunia Mwaka mmoja kabla Fainali zenyewe ili kupima
uwezo wao kuandaa Mashindano makubwa.
0 Maoni:
Post a Comment