WAPINZANI wa Jadi huko England, Manchester United na Liverpool
zinashuka Old Trafford Jijini Manchester kucheza Mechi muhimu ya EPL,
Ligi Kuu England.
Hii ni Mechi ya Mahasimu wakubwa Kihistoria huko England,
waliocheza Mechi yao ya kwanza kabisa Tarehe 28 Aprili 1894 wakati huo
Manchester United ikiwa na Jina lake la mwanzo kabisa Newton Heath,
Mechi ambayo ilibatizwa ‘Dabi ya Kaskazini-Magharibi’ ikizikutanisha
Timu zinazotoka Miji Miwili tofauti, Manchester na Liverpool, huko
Kaskazini Magharibi mwa England.
Man United wapo Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 5 nyuma ya Timu ya 4
Liverpool ambao wamefungana na Timu ya 3 Arsenal na wako Pointi 1 nyuma
ya Timu ya Pili Spurs na 8 nyuma ya Vinara Chelsea na zote hizi
zimecheza Mechi 1 zaidi kupita Man United na Liverpool.
Man United, chini ya Meneja Jose Mourinho, wanatinga Mechi hii
wakiwa na morali kubwa ya kushinda Mechi zao 6 zilizopita za EPL na pia
kutofungwa katika Mechi zao 15 zilizopita za Mashindano yote.
Liverpool, chini ya Meneja Jurgen Klopp, walitoka Sare Mechi yao ya
mwisho ya EPL na Sunderland 2-2 na pia Sare kwenye FA CUP na Plymouth
Argyle na kuchapwa 1-0 na Southampton kwenye Mechi ya Kwanza ya Nusu
Fainali ya EFL CUP.
Mechi hii ya Leo ni yao ya pili kwenye EPL Msimu huu baada kutoka 0-0 huko Anfield.
JE WAJUA KUHUSU MECHI HII?
Uso kwa Uso:
- Man United wameifunga Liverpool Mechi 79, Sare 53 na Kufungwa 65.
- Man United wametwaa Ubingwa wa England mara 20, mara ya mwisho ikiwa Mwaka 2013.
- Liverpool wametwaa Ubingwa wa England mara 18, mara ya mwisho ikiwa Mwaka 1990
Timu zote hizi zinaingia kwenye Mechi hii zikiwakosa Wachezaji wao
muhimu walioenda Gabon kushiriki AFCON 2017 kwa Man United kumkosa Beki
Eric Bailly ambae yuko na Timu ya Taifa ya Ivory Coast na Liverpool
kumpoteza Sadio Mane ambae yuko na Senegal.
Msimu uliopita kwenye Mechi kama hii iliyochezwa Old Trafford, Man United iliichapa Liverpool 3-1.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
MAN UNITED: DeGea, Valencia, Jones, Smalling, Blind, Fellaini, Herrera, Poga, Mkhitaryan, Ibrahimovic, Martial
LIVERPOOL: Mignolet, Clyne, Lovren, Matip, Milner, Wijnaldum, Henderson, Can, Lallana, Firmino, Coutinho
HUYU NDIYE REFA ATAKAYECHEZESHA MECHI HII.
Michael Oliver |
0 Maoni:
Post a Comment