POGBA ASEMA; MOURINHO ALINIAMBIA NIJISIKIE HURU NIKIWA UWANJANI.

Tokeo la picha la MOURINHO NA POGBA IMAGE
Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba anasema kuwa kuimarika kwa mchezo wake hivi karibuni kunatokana na mkufunzi wake Jose Mourinho kumwambia ajisikie ''huru uwanjani''.

Raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 alianza kuichezea klabu hiyo akiwa katika kiwango cha chini cha mchezo wake baada ya kujiunga na Manchester United.

Lakini amechangia pakubwa katika ushindi wa mechi tisa bila kushindwa wa Manchester United. 

''Aliniambia nisimsikize mtu yeyote ,nicheze mchezo wangu na kujifurahisha. Hivyo ndivyo nifanyavyo'', Pogba aliambia BBC. 

Tokeo la picha la POGBA IMAGE

''Pogba anacheza na motisha akituonyesha kitu anachoweza kufanya''. Kulikuwa na matumaini makubwa kufuatia kurudi kwa Pogba katika uwanja wa Old Trafford kutoka Juventus mnamo mwezi Agosti, lakini ni kuanzia hivi karibuni ambapo ushawishi wake katika timu hiyo umeanza kuonekana.

Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment