AFCON 2017 YAANZA KWA SARE KUTAWALA.

Tokeo la picha la gabon vs guinea bissau image afcon 2017

MASHINDANO ya 31 ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2017, yameanza Jumamosi Januari 14 huko Gabon kwa Wenyeji hao kuivaa washiriki wa mara ya kwanza kabisa Guinea-Bissau na kutoka nao Sare ya 1-1 katika Mechi ya Kundi A.
 
Bao la kusawazisha la Guinea Bissau lilifungwa Dakika ya 90 na Juary Soares wakati Gabon walitangulia kufunga Dakika ya 52 kwa Bao la Supastaa wao anaecheza Bundesliga huko Germany na Klabu ya Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang kumalizia Krosi ya Denis Bouanga.
Tokeo la picha la gabon vs guinea bissau image afcon 2017

Katika Mechi nyingine ya Kundi A iliyochezwa Jana, Burkina Faso na Cameroun nazo zilitoka 1-1 baada ya Cameroon kuongoza kwenye Dakika ya 35 kwa Frikiki ya Benjamin Moukandjo na Burkinabe kusawzisha Dakika ya 75 kupitia Issoufou Dayo aliemalizia Mpira wa Frikiki uliotemwa Na Kipa Fabrice Ondoa.

MAKUNDI:
KUNDI A: Gabon, Burkina Faso, Cameroon,       Guinea-Bissau
KUNDI B: Algeria, Tunisia, Senegal, Zimbabwe
KUNDI C: Ivory Coast, DR Congo, Morocco, Togo
KUNDI D: Ghana, Mali, Egypt, Uganda

Leo zipo Mechi 2 za Kundi B wakati Algeria wakicheza na Zimbabwe na kufuatiwa ile ya Tunisia na Senegal n azote kuchezwa huko Port Gentil Stadium, Port Gentil, Gabon.
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment