AFCON 2017: CHRISTIAN BASSOGOG MWANASOKA BORA

Tokeo la picha la Christian Bassogog image

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Cameroon, Christian Bassogog amechaguliwa kuwa Mwanasoka Bora wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika iliyomalizika nchini Gabon mwaka huu 2017.

Mchezaji huyo amekuwa msaada mkubwa kwa timu yake ya Cameroon kuweza kutwaa Kombe la AFCON, baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Misri kwenye mchezo wa fainali ambao ulipigwa katika dimba l'Amitie mjini Libreville na kutajwa kuwa Mchezaji Bora wa Mashindano na Kamati ya Ufundi ya CAF na kikundi cha Watathmini.

Orodha ya wachezaji wengine waliofanya vizuri katika michuano hiyo ni;  
  • Benjamin MOUKANDJO (Cameroon) Mchezaji bora, 
  • Tuzo ya Fair Play - Misri, 
  • Mfungaji Bora-Junior KABANANGA (DRC) Mabao 3, 
  • Kikosi cha Mashindano cha CAF - Kipa Fabrice ONDOA (Cameroon),Mabeki- Modou Kara MBODJI (Senegal), Ahmed HEGAZY (Misri), Michael NGADEU (Cameroon)
Viungo-Charles KABORE (Burkina Faso), Daniel AMARTEY (Ghana), Bertrand TRAORE (Burkina Faso), Christian ATSU (Ghana), Mohamed SALAH (Misri) .
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment