MASHINDANO
ya AFCON 2017, Kombe la Mataifa ya Afrika, Leo yanafika tamati huko
Nchini Gabon kwa Mechi ya Fainali kati ya Mabingwa wa Afrika mara 7
Egypt na Cameroon waliowahi kuutwaa Ubingwa mara 4.
Kwa
Egypt, hii itakuwa mara ya 4 mfululizo wakijaribu kubeba Ubingwa baada
ya kuutwaa Miaka ya 2006, 2008 na 2010 na kutofuzu Fainali za Miaka ya
2012, 2013 na 2015.
Fainali hii ni marudio ya Fainali ya Mwaka 2008 ambayo Egypt na Cameroon zilipambana.
Timu hizo zina Wachezaji kadhaa Maprofeshenali huko Ulaya na baadhi yao wapo huko Uingereza.
Cameroon
wanae Kiungo wa Hearts ya Scotland, Arnaud Djoum, na Clinton N'Jie,
ambae sasa yupo Marseille akitokea kwa Mkopo huko Tottenham.
Egypt
wanao Wachezaji Watatu wanaocheza EPL, Ligi Kuu England, ambao ni Beki
Ahmed Elmohamady (Hull City na Viungo Mohamed Elneny (Arsenal) na
Ramadan Sobhi (Stoke City), pamoja na Winga wa zamani wa Chelsea Mohamed
Salah ambae sasa yupo Italy Klabuni AS Roma.
Egypt
wametinga Fainali hii baada ya kuibwaga Burkina Faso 4-3 kwa Mikwaju ya
Penati kufuatia Sare ya 1-1 huku Shujaa wao akiwa Kipa mwenye Umri wa
Miaka 44 Essam El Hadary.
Cameroon,
wakiwa na Timu iliyobadilika baada ya Nyota wao kadhaa kugomea kujiunga
nao, wametinga Fainali kwa kuifunga Ghana, iliyopewa nafasi kubwa, 2-0.
0 Maoni:
Post a Comment