Emmanuel Frimpong raia wa Ghana amejiunga AFC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Sweden.
Frimpong anaungana na Mtanzania mwingine, Thomas Ulimwengu anayekipiga katika timu hiyo lakini anajaza nafasi aliyokuwa amewekewa Said Ndemla wa Simba.
AFC ilikuwa ikimtaka Ndemla lakini ilikuwa ikitaka kumchukua na baadaye akiuzwa, basi yenyewe na Simba wagawane.
Lakini hilo, lilionekana kutokubaliwa na viongozi wa Simba na sasa Frimpong anachukua nafasi yake baada ya kujiunga na AFC akitokea Arsenal Tula inayoshiriki Ligi Kuu ya Russia.
Kabla ya hapo, Frimpong alikuwa kiungo wa Arsenal ya England ambayo ilimpeleka kwa mkopo Wolveshampton, baadaye Charlton Athletic na Fulham.
Mwaka 2014 alijiunga Barnsley na baada ya hapo akaenda Ufa kabla ya kutulia Arsenal Tula akiwa na kiungo au beki wa zamani wa TP Mazembe, Stopilla Sunzu.
Tayari Frimpong ametambulishwa huku mmiliki wa AFC akishuhudia.
0 Maoni:
Post a Comment