JACK PEMBA AAMUA KUREJEA NA KUSAIDIA UWEKEZAJI WA MICHEZO NYUMBANI TANZANIA

PEMBA

Mtanzania Jack Pemba ameamua kurejea nchini kwa lengo la kuwekeza na kuisaidia michezo nchini.


Pemba ambaye wakati fulani aliwahi kujitokeza na kusaidia michezo lakini alidai kukosa sapoti, sasa ameamua kupitia moja kwa moja serikalini ili kupata ushirikiano sahihi.



Imeelezwa, Pemba yuko tayari kuingiza zaidi ya shilingi milioni 500 katika mchango wake katika masuala mbalimbali ya michezo lakini atajua kiasi gani hasa atoe baada ya kufanya mazungumzo na serikali.

Akizungumza na Championi Ijumaa, kaka wa Jack aitwaye Eliud Pemba amesema mdogo wake ameona ana kila sababu ya kusaidia nyumbani.



“Unajua amekuwa akisaidia mambo mengi ya michezo nchini Uganda. Ameona msaada huo unaweza kuwa jambo zuri katika michezo nchini ambapo hapa ni kwao.


“Jack anarejea Ijumaa (leo) anatokea Dubai, anakuja hapa na anatarajia kwenda kufanya mazungumzo na serikali kwa kuwa ameona upande wa wizara ya michezo, waziri ni mtu makini.


“Hivyo, anataka kutoa mchango wake na mimi nikiwa kaka yake na Mtanzania mwenzenu, nawaomba tumuunge mkono na kumpa moyo ili asaidiane na serikali kusaidia michezo,” alisema.



Pemba amechaguliwa kuwa rais wa mchezo wa kick boxing barani Afrika na imeelezwa pamoja na soka, riadha na michezo mingine, pia anahitaji maendeleo ya juu ya kick boxing. 
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment