Wakati
homa ya pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga ikizidi kupanda
taratibu, Kocha Msaidizi wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja, ametamka
kuwa hawana hofu hata kidogo na wapinzani wao hao huku wakiwaza mchezo
wao unaofuata dhidi ya African Lyon.
Vinara
hao wa ligi watawavaa wapinzani wao wakuu Yanga kwenye mechi ya ligi
itakayopigwa Februari 25, mwaka huu ambapo pambano hilo linatarajiwa
kuwa na ushindani kutokana na tofauti ya pointi baina ya timu hizo.
Mayanja
amesema hawawezi kuwafikiria Yanga kutokana na mchezo wao kuwa mbali na
kilichopo kwenye fikra zao ni kuangalia namna ya kulipa kisasi kwa Lyon
kwenye mechi ya Kombe la FA (Shirikisho), Alhamisi ijayo.
“Yanga
hatuna wasiwasi nao kwa sababu mechi yao ipo mbali lakini hata ikija
tutacheza kwa uwezo wetu kuhakikisha tunapata matokeo mbele yao na
tunaamini tunaweza kufanya hivyo.
“Lakini sasa tunaangalia namna ya kuwafunga Lyon kwenye mechi yetu inayofuata,” alisema Mayanja.
0 Maoni:
Post a Comment