Walau kidogo watu
wanaweza kupumua, hii ni baada ya taarifa kutoka kuwa mpiganaji Conor
McGregor na bondia Floyd Mayweather wanaonekana kukaribia kuingia
ulingoni.
Ingawa hakuna mkataba rasmi uliosainiwa, jarida la Irish Sun linaripoti
kuwa mpiganaji huyo kutoka kwenye kampuni ya upiganaji ya Ultimate
Fighting Championship (UFC) na bondia aliyestaafu wanaonekana kukaribia
kufikia makubaliano ya kiuchumi ili kufanya mchezo huo ufanyike ambao
utakuwa ndondi.
Ripoti inasema kuna upande wa tatu ambao unafanya
mkataba huo usisainiwe.
Kama tunaweza kumuamini rais wa UFC, Dana White mambo yanaweza kwenda mrama kati ya mapromota na mtukutu McGregor.
McGregor ama “Notorious” hajawahi kuficha kuwa siku zote anafanya mambo kwa misingi yake mwenyewe.
McGregor amekuwa
anatamani kupata hili pambano kwa udi na uvumba lakini likiwa na fedha
pia. Mwishoni mwa mwaka jana, McGregor alipata leseni ya kushiriki
mchezo wa ndondi katika jimbo la California. Lakini pia alitoa video
zilizomuonyesha kifanya mazoezi ya ubondia maarufu kama Sparring.
Mayweather siku zote
amekuwa muwazi kuwa haogopi kupigana na “Notorious.” Katika siku za
karibuni alimwambia Jim Gray kwenye mahojiano maalumu kuwa mpambano wake
na McGregor upo kwenye hatua za mwisho za kuiva.
Mpambano wa mwisho wa
McGregor ulikuwa dhidi ya Eddie Alvarez kwenye UFC 205 ndani ya Madison
Square Garden huko katika jiji la New York. “Notorious” alimpiga Alvarez
ukiwa ni ushindi wake wa pili wa TKO. Ushindi huo
ulimfanya McGregor kuwa mtu wa kwanza kushinda mikanda miwili ya UFC kwa
nyakati zilizofuatana.
Mayweather ameonekana ulingoni mara ya mwisho Sept. 2015.
0 Maoni:
Post a Comment