Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Mesut Ozil anaamini analaumiwa bila msingi wowote kutokana na matatizo yanayoikumba klabu hiyo, wakala wake amesema.
Ozil, 28, alilaumiwa tena baada ya Arsenal kupokezwa kichapo cha 5-1 ugenini kwa Bayern Munich katika mechi ya hatua ya 16 bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya siku ya Jumatano.
"Ukosoaji ni kawaida mchezaji anapocheza vibaya," Dkt Erkut Sogut aliiambia BBC Sport.
"Lakini Mesut anahisi kwamba watu hawaangalii vyema uchezaji wake; na badala yake analaumiwa bure baada ya timu kupata matokeo mabaya."
Ozil alijiunga na Arsenal kutoka Real Madrid mwaka 2013 kwa ada ya £42.4m iliyovunja rekodi ya klabu hiyo ya England.
Alitua Emirates akiwa na sifa za kuwa mmoja wa viungo wa kati wazuri sana duniani
Lakini uchezaji wake karibuni umekosolewa sana.
Dhidi ya Bayern, alikamilisha pasi 20 pekee, ambazo ni sawa na alizokamilisha kipa wa Bayern Manuel Neuer.
"Bayern walidhibiti mpira 74% ," alisema Sogut, ambaye pia ni wakili wa Ozil.
"Mchezaji ambaye ni nambari 10 uwanjani anawezaje kuunda nafasi iwapo hapati mpira?
"Katika mechi kama hizi watu humlenga zaidi mchezaji aliyegharimu pesa nyingi na anayelipwa pesa nyingi - na huyo ni Ozil. Lakini hawezi kulaumiwa kila wakati. Si haki.
"Soka ni mchezo wa timu na Arsenal kwa sasa hawachezi vyema kama timu. Kulikuwa na wachezaji kumi na mmoja uwanjani lakini Mesut ndiye anayelaumiwa. Je, ndiye aliyesababisha Arsenal kufungwa magoli matano?" TOA MAONI YAKO BAADA YA KUISOMA HII HABARI
0 Maoni:
Post a Comment