Unaweza
kusema ni kiroho safi Mtibwa Sugar imesema kipigo cha mabao 5-0
walichopata kutoka kwa Mbao FC juzi Alhamisi kwenye Ligi Kuu Bara ni
haki yao na wala hakuna wa kumtupia lawama.
Ikicheza
kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Mtibwa ilikubali kipigo hicho
kutoka kwa Mbao ambayo imepanda msimu huu kucheza ligi kuu. Hicho ni
kipigo cha pili kwa Mtibwa kutoka timu za Kanda ya Ziwa kwani mwanzoni
mwa wiki hii, walifungwa mabao 2-0 na Kagera Sugar.
Ofisa
Habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru, ameliambia Championi Jumamosi kuwa:
“Ama kweli kipigo tulichokipata kutoka kwa Mbao ni halali yetu, hatuwezi
kumlaumu mtu yeyote wa nje, waamuzi wamefanya kazi yao ipasavyo,
wanahitaji pongezi.
“Tumekumbana
na dhoruba kali sana, Mbao walistahili ushindi kwa sababu hatujacheza
kwa kiwango chetu kile cha kawaida, lakini kipigo hicho kimetufanya
tujipange kikamilifu kwa ajili ya mchezo wetu ujao dhidi ya African
Lyon, tunawaahidi mashabiki wa Mtibwa hatutarudia makosa.”
Baada
ya kipigo hicho, Mtibwa imebaki katika nafasi ya tano na pointi zake 31
katika mechi 21 ilizocheza ikiwa imefunga mabao 23 na kufungwa 26.
0 Maoni:
Post a Comment