Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017 uliendelea usiku wa Jumanne ya December 13 2016 kwa michezo miwili kupigwa, AFC Bournemouth waliwakaribisha Leicester City wakati Everton waliwakaribisha Arsenal katika uwanja wao wa Goodson Park.
Usiku wa December 13 Arsenal wakiwa ugenini kucheza mchezo wao wa 16 wa Ligi Kuu England wamekubali kupoteza kwa goli 2-1, magoli ya Everton yakifungwa na Seamus Coleman dakika ya 44 na Ashley Williams dakika ya 86 wakati goli la Arsenal limefungwa na Alex Sanchez dakika ya 20.
Huu unakuwa mchezo wa pili wa Ligi Kuu England kwa Arsenal kupoteza msimu huu, Arsenal wameshindwa kutoka na ushindi Goodson Park kwa mara ya tatu mfululizo, mara ya mwisho Arsenal alicheza na Everton katika uwanja huo March 19 2016 na kupata ushindi wa goli 0-2.
0 Maoni:
Post a Comment