Jose Mourinho ameeleza kuwa sasa yupo na furaha akiwa na Manchester United na imekuwa rahisi kwake kujisikia Nyumbani kwa Klabu hiyo ambayo ni moja ya Klabu kubwa Duniani.
Mourinho,
ambae ametua Man United mwanzoni mwa Msimu huu, alianza vizuri kwenye
EPL, Ligi Kuu England, lakini baadae wakayumba na sasa wamerudi kwenye
Reli na wapo Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 3 nyuma ya Timu ya 5 Tootenham,
Pointi 4 nyuma ya Arsenal walio Nafasi ya 4, Pointi 6 nyuma ya City
ambao ni wa 3, Pointi 7 nyuma yaw a 2 Liverool na 13 nyuma ya Vinara
Chelsea.
Akiongea
na Wanahabari kuelekea Mechi yao ya Jumatatu na Sunderland, Mourinho
amesema: “Watu wanataka kuwa na furaha tena…Watu wana matumaini makubwa
ingawa kwa sasa hatupo nafasi nzuri!”
Jumatatu,
Uwanjani Old Trafford, Man United itacheza na Sunderland ambayo iko
Nafasi ya 18 na wapo chini ya Meneja wa zamani wa Man United David Moyes
ambae alimrithi Lejendari Sir Alex Ferguson Mwaka 2013 na kutimuliwa
Miezi kadhaa baadae.
Mourinho, ambae sasa ameiongoza Man United kwenye Mechi 10 bila kufungwa, ametoboa kuwa hajawahi kuongea na Moyes.
Mourinho pia aliponda Ratiba ya EPL kwa kipindi hiki cha Krismasi na Mwaka Mpya na kudai baadhi ya Klabu zimependelewa.
Ameeleza:
“Kipindi hiki kigumu cha Mechi mfululizo, Chelsea wako na Ratiba
nyepesi isiyokuwa msongamano. Sie tofauti lakini tumezoea kwani tuko
Europa Ligi!”
************************************************************************
0 Maoni:
Post a Comment