Mchezo kati ya Manchester City na Chelsea uliisha kwa ushindi kwenda upande wa Chelsea. Lakini timu zote mbili zilionyesha utovu wa nidhamu na kusababisha baadhi ya wachezaji wa timu hizi kutolewa nje.
Baada ya kupitia mchezo huo, F.A imezipiga faini club zote mbili kiasi cha Pound 35,000 kwa Manchester City na Pound 100,000 kwa Chelsea. Ilikua inazungumzwa kwamba club hizi mbili zingepitia panga la kukatwa points lakini F.A imeachana na hiyo adhabu.
Hasa kwa Chelsea ambayo imekua ni mara ya tano ndani ya miezi 18ikikubali kukutwa na makosa ya aina hiyo. Swala hili ndilo lilikua linaleta mashaka ya labda Chelsea ingeweze kukumbwa na hili panga.
Club hizi zinatarajiwa tena kukutana ikifika April 5 kwenye mechi ya pili ya ligi kuu ya England.
0 Maoni:
Post a Comment