Kijana Bradley Lower ni shabiki mkubwa wa klabu ya Sunderland. Bahati mbaya ni kuwa pamoja na mapenzi yake makubwa ya mchezo huu, maisha yake yapo hatarini kutokana na kusumbuliwa na maambukizi ya saratani ambayo yanasemekana kufika hatua ambayo yanaweza yasitibike.
Ulimwengu wa wapendasoka duniani hasa mashabiki wa soka wameungana katika kumuunga mkono kijana huyu mwenye umri wa miaka 5 ili aendelee kupigania maisha yake baada ya kusemekana amebakisha muda mfupi wa kuishi duniani.
Bradley Lowery,ambaye anatokea Blackhall Colliery jirani kabisa na Hartlepool, alibainika kuwa na saratani inayofahamika kama Neuroblastoma mwaka 2013.
Zaidi ya paundi laki 7 (£700,000) ambayo ni zaidi ya bilioni mbili za Kitanzania zimeshakusanywa kuweza kumsaidia kwenda kutibiwa Marekani baada ya taarifa za awali kusema hawezi kutibiwa Uingereza huku klabu ya Everton ikiahidi kutoa paundi laki mbili (£200,000.)
Baada ya miaka miwili ya mateso kutokana na ugonjwa huu, mtoto huyu alifanyiwa matibabu “chemotherapy” na ilisemekana kuwa amepona ugonjwa huo na akaendelea kuishi maisha yake ya kawaida kwa kipindi cha miezi 18 kabla haijathibitika ugonjwa huo kurejea tena mwezi Juni mwaka huu.
0 Maoni:
Post a Comment