Siku zote mapenzi juu ya kitu fulani huwa hayajifichi. hii inathibitishwa na aliyekuwa kocha wa Azam fc Stewart hall na mapenzi yake juu ya club ya Azam. Kocha mkuu wa klabu ya AFC Leopards, Stewart Hall amezungumzia kufukuzwa kwa benchi la ufundi la klabu yake ya zamani ya Azam.
Katika mazungumzo na mtandao wa www.kiungomshambuliaji.blogspot.com, Hall amefurahishwa na uamuzi wa kumrejesha Kally Ongala kuchukua mikoba ya Wahispania.
Anasema hivi ” Ni maamuzi sahihi, nadhani Kally atawafaa sana, namuunga mkono. ”
Hall alimsajili Kally kama kocha-mchezaji pamoja na kumpa majukumu ya ukocha msaidizi kabla ya wote kuondoka baada ya Kally kuamua kwenda kusomea ukocha Uingereza huku Hall akijiuzulu.
Katika mazungumzo ya huko nyuma na mtandao wa www.kiungomshambuliaji.blogspot.com, Hall alisema anaumizwa mno na matokeo mabovu ya Azam kwani ni timu ambayo anaipenda na yuko tayari kurudi kuifundisha.
0 Maoni:
Post a Comment