Southampton imewatandika Bao 4-1 na TOTTENHAM katika Mechi pekee ya EPL, Ligi Kuu England, iliyochezwa Jana Usiku huko Uwanja wa Saint Mary huku Dele Alli akipiga Bao 2.
Ni Southampton, maarufu kama ‘Watakatifu’, ndio waliotangulia kufunga katika Dakika ya Pili tu pale Virgil Van Dijk alipopiga Kichwa na kuunganisha Frikiki ya James Ward-Prowse.
Spurs wakasawazisha Dakika ya 19 kupitia Dele Alli alieunganisha Krosi ya Moussa Dembele.
VIRGIL VAN DIJK |
Kipindi cha Pili, Dakika ya 52, Harry Kane akawapa Spurs Bao la Pili kwa Kichwa kufuatia Kona ya Christian Eriksen.
Watakatifu
wakabaki Mtu 10 Dakika ya 57 Nathan Redmond alipopewa Kadi Nyekundu kwa
kumchezea Rafu Alli na Refa Mike Dean kutoa Penati ambayo Kane
alipaisha.
Pengo
hilo liliwapa mwanya Spurs kutawala na kuongeza Bao 2 kwenye Dakika za
85 na 87 Wafungaji akiwa Son Heung-Min na Alli na mwishowe kushinda 4-1.
Spurs
wanabaki Nafasi ya 5 kwenye EPL lakini sasa pengo lao na Timu ya 4
Arsenal ni Pointi 1 tu na pia kuiacha Timu ya 6 Man United Pointi 3
nyuma.
Southampton wapo Nafasi ya 8 wakiwa Pointi 12 nyuma ya Spurs.
VIKOSI:
SOUTHAMPTON: Forster, Cedric, Van Dijk, Fonte, Bertrand, Ward-Prowse, Davis, Romeu, Boufal, Redmond, Rodriguez
Akiba: Taylor, Yoshida, Long, Tadic, Martina, Reed, Hojbjerg.
TOTTENHAM: Lloris, Walker, Dier, Vertonghen, Rose, Wanyama, Dembele, Sissoko, Eriksen, Dele, Kane
Akiba: Vorm, Davies, Wimmer, Winks, Nkoudou, Son, Janssen
REFA: Mike Dean
0 Maoni:
Post a Comment