MCHEZAJI WA UHOLANZI Memphis Depay amesema hakuwa na uhusiano mbaya na Jose Mourinho licha ya kucheza kwa nadra chini yake.
Depay,
mwenye Miaka 22, aliihama Man United Wiki iliyopita na kujiunga na
Lyon ya France baada ya kukosa namba kwenye Kikosi cha Mourinho.
Depay
alicheza Dakika 20 tu za Mechi za EPL, Ligi Kuu England, Msimu huu na
kuuzwa kwa Lyon Wiki iliyopita kwa Dau la Pauni Milioni 21.7 kwa Mkataba
ambao una Kipengele cha Man United kumnunua tena ikiwa atatoswa huko
Lyon.
Alipoondoka, Jose Mourinho, aliweka wazi milango kurejea tena kwa Depay kwa vile si ‘Mchezaji mbaya’.
Nae
Depay, akiongea na OL TV na kuonyesha hana kinyongo kabisa na Mourinho
kuhusu kuuzwa kwake, alitamka: “Maneno yake yalikuwa ni mazuri. Kule
Manchester nilifanya bidii lakini nataka kucheza kila Mechi. Hatukuwa na
uhusiano mbaya!”
Aliongeza: “Ni Kocha mzuri na Mtu mwema!”
Wikiendi iliyopita, Depay aliichezea Mechi yake ya kwanza Lyon akiingizwa kutoka Benchi na Timu yake kuichapa Marseille 3-1.
Depay,
ambae huichezea Timu ya Taifa ya Netherlands, amefunga Bao 7 kwa Man
United katika Mechi zake 53 alizocheza tangu ajiunge kutoka PSV
Eindhoven Mei 2015 kwa Dau la Pauni Milioni 25.
Msimu huu, Depay ameichezea Man United Mechi 8 tu lakini tangu Oktoba amecheza Dakika 8 tu.
Katika
kipindi hiki cha Dirisha la Uhamisho la Januari, Depay amekuwa Mchezaji
wa Pili kuuzwa na Man United na mwingine ni Morgan Schneiderlin
alieuzwa kwa Everton Januari 12 kwa Ada ya Pauni Milioni 24.
0 Maoni:
Post a Comment