MCHEZAJI
wa zamani wa Manchester United Patrice Evra anatarajiwa
kuichezea Timu yake mpya huko kwao France Marseille wakati
wakiikaribisha Montpellier kwenye Mechi ya Ligi 1.
Evra,
mwenye Miaka 35, ameihama Juventus na kurejea kwao France kujiunga na
Marseille ambayo sasa inaimarishwa vilivyo na Mmiliki wake kutoka
Marekani, Frank McCourt, ambae ashamsimika Kocha Mpya Rudi Garcia na
yupo kwenye harakati kubwa kumsaini Mchezaji wa Kimataifa wa France
anaechezea West Ham Dimitri Payet.
Akiongelea
kuhusu kuondoka kwa Evra, Kocha wa Juventus Massimiliano Allegri
ametamka: “Ni Bingwa mkubwa, Mchezaji wa Kulipwa mwenye kila kitu!”
Hivi sasa Marseille wapo Nafasi ya 7 wakiwa Pointi 15 nyuma ya zile Nafasi za Timu kuichezea UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Mbali
ya mvuto huo wa Evra, Ligi 1 itavutia zaidi hapo Jumapili wakati
Mabingwa Watetezi Paris Saint-Germain wakiwavaa Vinara wa Ligi hiyo kwa
sasa AS Monaco.
Baada
ya kumnasa Julian Draxler Siku ya Mwaka Mpya, PSG watamkaribisha
Straika wa Portugal mwenye Miaka 20 kutoka Benfica Goncalo Guedes.
AS Monaco wanaongoza Ligi 1 wakiwa na Pointi 48 wakifuata Nice wenye Pointi 46 na PSG ni wa 3 wakiwa na Pointi 45.
France -LIGI 1
RATIBA
Leo Ijumaa Januari 27
Marseille v Montpellier
Jumamosi Januari 28
Lyon v Lille
Angers v Metz
Bastia v Caen
Lorient v Dijon
Nancy v Bordeaux
Rennes v Nantes
Jumapili Januari 29
Nice v Guingamp
Toulouse v Saint Etienne
Paris Saint-Germain v Monaco
0 Maoni:
Post a Comment