Pamoja na kupoteza mechi ya fainali dhidi ya Azam FC na kuukosa ubingwa, Bosi Msaidizi wa benchi la ufundi la Simba, Jackson Mayanja
ameibuka na kusema kuwa, michuano ya Kombe la Mapinduzi imewasaidia
kuwajenga na kuwapatia kikosi bora kitakachopambana kutwaa ubingwa wa
Ligi Kuu Bara.
Michuano
ya Kombe la Mapinduzi imefikia tamati jana kwa kuzikutanisha Simba na
Azam ambapo Azam FC iliibuka na ushindi wa bao 1-0 na kumaliza
mashindano bila ya kufungwa mechi wala bao hata moja.
Mayanja
alisema michuano hiyo imewasaidia katika kukiimarisha kikosi chao kwa
lengo la kufanikisha mikakati yao ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu.
“Tatizo
letu kubwa katika kikosi chetu ni safu ya ushambuliaji hasa katika
suala zima la umaliziaji, hivyo tumetumia muda huu kukijenga vyema kwa
kikosi kuhakikisha tunafanikiwa kupata mabao ya mapema.
“Naamini
iwapo tutapata mabao ya harakaharaka ambayo ndiyo yatakayotuweka katika
nafasi nzuri zaidi ya ushindi, michuano hii imesaidia kujenga kikosi
chetu na kubaini makosa mbalimbali.
“Mwisho
wa siku tutaweza kufanikiwa kutwaa ubingwa hivyo naamini kila mchezaji
atakuwa ametoka na nguvu mpya katika michuano hii.
“Mara
baada ya kumaliza michuano hii akili zetu zote tunazielekeza kwenye
ligi ambapo lengo letu kubwa ni kuona tunafanikiwa kutwaa ubingwa,”
alisema Mayanja.
0 Maoni:
Post a Comment