AZAM FC YAWEKA REKODI MPYA MAPINDUZI CUP BAADA YA KUIFUNGA SIMBA SC.



Azam FC imefunga Simba kwa bao 1-0 katika mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.

Kwa Ushindi huo, Azam FC wanakuwa mabingwa Mapinduzi 2017 lakini wanaweka rekodi ya kubeba kombe hilo bila ya kupoteza mchezo wala kufungwa hata bao moja.


Azam FC imeishinda Simba katika mchezo safi na kufanikiwa kubeba kombe hilo mara tatu sawa na Simba ambayo pia imewahi kulibeba mara tatu, huku mabingwa wengine kama Yanga na Mtibwa Sugar wakiwa wamewahi kulibeba kombe hilo mara moja tu.
 http:// kiungomshambuliaji.blogspot.com
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment