Kiungo
mwenye kasi wa Yanga, Simon Msuva amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo
kwa kuwaambia wanaanza rasmi mbio za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara
kwa kukutana na Majimaji.
Kauli
hiyo ya Msuva imekuja baada ya timu hiyo kulikosa taji la ubingwa wa
Kombe la Mapinduzi ambayo Yanga iliondolewa na Simba kwenye hatua ya
nusu fainali.
Yanga, wanatarajiwa kupambana na Majimaji, Januari 17, mwaka huu mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Majimaji mkoani Songea.
Msuva
alisema mashabiki wasikate tamaa baada ya kulikosa Kombe la Mapinduzi
na badala yake wanachotakiwa kukifanya ni kuungana kwa pamoja ili
wautetee ubingwa wao wa ligi kuu.
Msuva
alisema michuano hiyo waliichukulia kama sehemu ya maandalizi ya ligi
kuu, hivyo haumizwi na kuukosa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi.
Alisema
michuano hiyo imewasaidia kujua upungufu wa kikosi chao ambao Kocha
George Lwandamina kwa kushirikiana msaidizi wake Juma Mwambusi
wataufanyia marekebisho ili wapate matokeo mazuri katika ligi.
“Ninaamini kocha amejua upungufu wa kikosi chetu baada ya kuondolewa na Simba kwenye nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi.
“Hicho
ndicho tulichokuwa tunakihitaji kwa kupitia Kombe la Mapinduzi ni kujua
upungufu wetu ambao kocha ataufanyia marekebisho kwa kuziboresha sehemu
zenye upungufu tukijiandaa kucheza na Majimaji.
“Mashabiki
wa Yanga wanatakiwa kuachana na maneno ya kejeli na vijembe
wanayoyapata kutoka kwa wapinzani wetu, nikwambie tu tumepanga kulitetea
taji letu la ligi kuu,” alisema Msuva.
0 Maoni:
Post a Comment